المستخلص: |
تتناول هذه الدراسة موضوع اللواصق الصرفية في اللغة السواحيلية لتحديد وظيفتها الصرفية والفرق بينها، وبدأت الدراسة بمقدمة تناول فيها الباحث مفهوم مصطلح علم الصرف وتاريخ استخدامه وأنواعه وشرح بعض المصطلحات المتعلقة بموضوع البحث، ثم قام الباحث بتحليل مادة البحث والتي اعتمد في تحليلها على أسس النظرية الصرفية الدلالية، وقد خلصت الدراسة إلى إمكانية التمييز بين نوعين من اللواصق، النوع الأول هو اللواصق التي عندما تضاف إلى جذور الكلمات تعطينا معنى جديدا دون تغيير نوع الكلمة فإذا كانت الكلمة اسما. تبقى اسما، وإذا كانت فعلا فإنها تظل فعلا، وإذا كانت صفة فإنه تظل صفة، وهذا النوع من اللواصق يعرف باللواصق التصريفية. ومن خلال نتائج التحليل خلصت الدراسة إلى تعريف هذا النوع من اللواصق الصرفية بأنها لواصق تصريفية تضاف إلى جذور الكلمات فتعطينا معنى جديدا دون أن تغيير نوع الكلمة أما بالنسبة للنوع الثاني من اللوصق عند إضافتها إلى جذور الكلمات، فإنها تتقوم بتغيير معنى الكلمة ونوعها، أي أن الكلمة قبل إضافة اللاصقة يمكن أن تكون اسما، وبعد إضافتها تصبح فعلا.، ويمكن أن تكون صفة وبعد إضافة اللاصقة تصبح فعلا. وقد خلصت الدراسة إلى تعريف هذا النوع من اللاوصق الصرفية بأنها لواصق اشتقاقية عندما تضاف إلى جذور الكلمات تقوم بتغيير معنى ونوع الكلمة فتنقل الكلمة من حقل دلالي إلى حقل دلالي آخر.
Utafiti huu unashughulikia suala la viambishi vya mofolojia katika Kiswahili ili kubainisha tofauti kati ya viambishi hivi. Utafiti ulianza na utangulizi ambapo mtafiti alishughulikia dhana ya istilahi mofolojia, historia ya matumizi yake na aina zake, Utafiti ulitegemea nadharia ya Mofolojia Leksia kwa Uchambuzi wa data.Utafiti ulihitimisha kuwa tunaweza kutofautisha aina mbili za viambishi.Aina ya kwanza ni viambishi ambavyo huongezwa kwenye mzizi wa neno hivyo kutupa maana mpya bila kubadilisha aina ya neno maana ikiwa neno ni nomino., hubakia kuwa nomino, na ikiwa ni kitenzi, hubakia kuwa kitenzi, na ikiwa ni kivumishi, hubakia kuwa kivumishi, aina hii ya viambisi inaitwa viambishi vya unyambulishaji wa maneno. Tunaweza kufafanua aina hii ya viambishi vya kimofolojia kwamba ni: viambishi vya unyambulishaji wa maneno vilivyoongezwa kwenye mizizi ya maneno, kutupa maana mpya bila kubadilisha aina ya neno. Ama aina ya pili ya viambishi vinapoongezwa kwenye mzizi wa neno hubadilisha maana na aina ya neno, yaani neno kabla ya kuongeza kiambishi huweza kuwa nomino, baada ya kuongezwa huwa ni kitenzi., na inaweza kuwa kivumishi, na baada ya kuongeza inakuwa kitenzi, lakini pia si lazim tunapoongezwa viambishi hivi tunapata neno jipya. Na tunaweza kufafanua aina hii ya viambishi vya kimofolojia kama ifuatavyo: Viambishi vya uundaji wa maneno vinavyoongezwa kwenye mizizi ya maneno, hivyo kutupa neno jipya lenye maana mpya tofauti na neno la kwanza, hivyo basi kuhamisha neno kutoka uwanja mmoja wa kisemantiki hadi uwanda mwingine wa kisemantiki.
|